Mark 14:53-58

53 aWakampeleka Isa kwa kuhani mkuu, nao viongozi wa makuhani wote, na wazee na walimu wa sheria wote wakakusanyika pamoja. 54 bPetro akamfuata kwa mbali, hadi uani kwa kuhani mkuu. Huko akaketi pamoja na walinzi, akiota moto.

55 cViongozi wa makuhani na Baraza la Wayahudi
Baraza la Wayahudi hapa ina maana ya Sanhedrin ambalo lilikuwa ndilo baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi, lililoundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.
lote wakatafuta ushahidi dhidi ya Isa ili wapate kumuua. Lakini hawakupata jambo lolote.
56Wengi walitoa ushahidi wa uongo dhidi yake, lakini maelezo yao hayakukubaliana.

57Ndipo wengine wakasimama wakatoa ushahidi wa uongo dhidi yake, wakisema: 58 e“Sisi tulimsikia akisema, ‘Mimi nitalibomoa Hekalu hili lililojengwa na wanadamu, na katika siku tatu nitajenga jingine ambalo halikujengwa na wanadamu.’ ”
Copyright information for SwhKC